Pages

Ads 468x60px

Featured Posts

Sunday, June 22, 2014

PICHA ZA SHOW YA DIAMOND SONGEA



 Jana ilikuwa ni mwendelezo wa tou
r za music,Kili music
 tour kwa washindi wa tuzo za KTMA na baadhi y
a wasanii,kutokana na ratiba kubana
 ikiwemo MTV awards,sikuweza kushiriki show za mwanzo,hii ya Songea imekua ya kwanza,nishukuru watu wangu wa Songea kwa sapoti
 kubwa waliyoitoa kwangu na wasanii wenzangu wote
 walioshiriki ..hizi ni baadhi ya picha ilivyokuwa.



















Tuesday, June 17, 2014

MAPOKEZI YA WASANII SONGEA KWA AJILI YA KILI TOUR SONGEA


 Juni 15, 2014 majira ya mchana kulikuwa na mapokezi ya wasanii wanaowasha moto katika Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 linalofanyika Uwanja wa Maji Maji mjini Songea. Hapa walikuwa wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Songea.
 Wasanii Ommy Dimpoz na Shilole wakiwasili mjini Songea kwa ajili ya Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 linalofanyika Uwanja wa Maji Maji.
 Hata mimi nilipata nafasi ya kushow love na Msanii Diamond Platinumz mara baada ya kuwasili mjini Songea.
 Wasanii Ben Pol na G-Nako wakipata ukodak.
 Showlove kwa Mama Khadija Kopa, Diamond na Mwasiti.
 Diamond akitoka Uwanja wa Maji Maji Songea.
 Malkia wa Mipasho, Mama Khadija akitoka Uwanjani mara baada ya kuwasili mjini Songea.
 Wapenzi wa Ommy Dimpoz wakipata nae ukodak.
 Wasanii walipata wasaa wa mahojiano kutoka Jogoo Fm ya Mjini Songea.

Tuesday, April 29, 2014

FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI‏

 Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi

Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.

  

         


Sunday, October 27, 2013

MTU MZIMA MATONYA BADO YUPO RUMANDE SONGEA...


 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Seif Shaban maarufu kama Matonya bado anaendelea kusota rumande mjini Songea baada ya kukataliwa dhamana kutokana na kufanya utapeli baada ya kulewa kupita kiasi na kushindwa kufanya shoo iliyoandaliwa na promota mmoja mjini humo.....

 

Matonya alitakiwa kufanya shoo kwenye Ukumbi wa Jambolee uliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Matonya alifika ukumbini akiwa amelewa hali iliyompelekea kushindwa kufanya show na kusababisha hasara katika ukumbi baada ya kufanya fujo ya kuvunja vitu ukumbi hapo, Ndipo waandaaji wa show hiyo walipoamua ifanyike kesho yake na kiingilio kiwe ni kununua bia .

Wakati huo msanii huyo alitakiwa akafanye show nyingine Wilaya ya Mbinga ambayo ilikuwa ni sehemu ya mkataba wao lakini hakufanya hivyo na matokeo yake akaamua kukata tiketi kurudi Dar es Salaam. Baada ya kuvuja taarifa hizo walimfata hadi alipokuwa amefikia na kukuta amehamia sehemu nyingine.

jokate aipeleka kidoti songea

photo(1)


photo(2)photo(4)