Pages

Sunday, June 22, 2014

PICHA ZA SHOW YA DIAMOND SONGEA



 Jana ilikuwa ni mwendelezo wa tou
r za music,Kili music
 tour kwa washindi wa tuzo za KTMA na baadhi y
a wasanii,kutokana na ratiba kubana
 ikiwemo MTV awards,sikuweza kushiriki show za mwanzo,hii ya Songea imekua ya kwanza,nishukuru watu wangu wa Songea kwa sapoti
 kubwa waliyoitoa kwangu na wasanii wenzangu wote
 walioshiriki ..hizi ni baadhi ya picha ilivyokuwa.



















Tuesday, June 17, 2014

MAPOKEZI YA WASANII SONGEA KWA AJILI YA KILI TOUR SONGEA


 Juni 15, 2014 majira ya mchana kulikuwa na mapokezi ya wasanii wanaowasha moto katika Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 linalofanyika Uwanja wa Maji Maji mjini Songea. Hapa walikuwa wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Songea.
 Wasanii Ommy Dimpoz na Shilole wakiwasili mjini Songea kwa ajili ya Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 linalofanyika Uwanja wa Maji Maji.
 Hata mimi nilipata nafasi ya kushow love na Msanii Diamond Platinumz mara baada ya kuwasili mjini Songea.
 Wasanii Ben Pol na G-Nako wakipata ukodak.
 Showlove kwa Mama Khadija Kopa, Diamond na Mwasiti.
 Diamond akitoka Uwanja wa Maji Maji Songea.
 Malkia wa Mipasho, Mama Khadija akitoka Uwanjani mara baada ya kuwasili mjini Songea.
 Wapenzi wa Ommy Dimpoz wakipata nae ukodak.
 Wasanii walipata wasaa wa mahojiano kutoka Jogoo Fm ya Mjini Songea.

Tuesday, April 29, 2014

FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI‏

 Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi

Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.